Bohari ya Dawa Tanzania yachangia Dawa Zenye Thamani ya Tsh. 1,265,465 kwa Taasisi ya Safe Haven kwa ajili ya Kituo cha Huduma ya Utengamao cha Antonia Verna

Mnamo siku ya Jumanne, 4 Julai, 2023 Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Save Haven yenye usajili namba 00/NGO/R/2963, iliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD) yenye dhumuni la kuomba msaada wa dawa zinazohitajika katika kituo cha Antonia Verna Community Based Rehabilitation kuwasaidia watoto wenye ulemavu 254, wenye matatizo yanayohusiana na Uti wa Mgongo, Utindio wa Ubongo, Usonji, Kupooza, na Ugonjwa wa Kupooza kwa Ubongo.

Antonia Verna Rehabilitation Centre ni kituo ambacho kinahudumia watoto wenye ulemavu na wanatoka katika kaya/familia zinazoishi katika mazingiza magumu kiuchumi kuwahudumia watoto hao.

Mnamo tarehe  21 Juni, 2023 tulitembelea kituo hicho cha Huduma ya Utengamao (Rehabilitation Centre) kujionea hali halisi ya kituo na mahitaji wanayohitaji. Kutokana na hali tuliyoiona na mahitaji yanayohitajika ndipo tuliamua kumuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) yenye orodha ya dawa muhimu zinazohitajika katika kituo kuwahudumia watoto wenye uhitaji.

Leo Alhamisi 13 Julai, 2023 tuliweza kupokea dawa aina ya Carbamazepine 200mg na Sodium Valproate 500mg zote kwa pamoja zina Jumla ya Shilingi Milioni Moja Laki Mbili Sitini na Tano Elfu na Mia Nne Sitini na Tano (1,265,465/-).

Tunapenda kumshukuru Mkurengezi wa Bohari ya Dawa (MSD) pamoja na Wafanyakazi wote kwa Msaada huu walioutoka kuwasaidia Watoto 254 kwa Kituo cha hicho cha Huduma ya Utengamao cha Antonia Verna.