Safe Haven Foundation, Samatta Foundation na Uratibu wa Maendeleo ya Uturuki (TiKA) Tanzania Yaadhimisha Miaka 100 ya Jamuhuri ya Uturuki

Safe Haven Foundation na Samatta Foundation tumeshirikiana na Taasisi ya Ushirikiano na Uratibu wa Maendeleo ya Uturuki (TiKA) Tanzania katika kuadhimisha Miaka 100 ya Jamuhuri ya Uturuki kwa kuzindua ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa kisasa katika Shule ya Msingi Msimbazi Mseto.

Tunamshukuru Mheshiwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Jomary Satura kwa kukamilisha shughuli kama mgeni rasmi.