Safe Haven Foundation yafanya mjadala maalum kwa vijana siku ya Jumapili, 21 Julai 2024 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana. Mjadala huu maalum wa Kijana Jasiri ulidhaminiwa na Benki ya CRDB na ulihidhuriwa na vijana 50 kutoka sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Mjadala ulifanyika katika Shule Ya Sekondari Makumbusho. Na tunapenda kutoa shukarini kwa vijana wote walishiriki mjadala huu mzuri.
Safe Haven Foundation ni shirika lisilotengeneza faida lenye usajili namba 00/NGO/R/2963 linalopatikana Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar Free Market Shopping Mall, Kinondoni ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, lenye kusudi la kutoa elimu pana ya afya ya uzazi kwa vijana balekhe Tanzania. Tumekuwa watetezi wakubwa katika kuhakikisha elimu sahihi ya afya uzaziinaelekezwa kwa vijana balekhe kusaidia maendeleo ya jamii kwa ujumla kupitia kundi hilo.