Safe Haven Foundation Yagawa Maboksi 100 ya Pedi (Sawa na Pedi 24,000) Kwenda Ofisi Binafsi ya Waziri ya Afya kwa ajili ya Watoto wa Kike Wanaoishi Katika Mazingira Magumu

Katika kuhakikisha tunawafikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, tulichangia jumla ya boksi 100 za taulo za kike na kuzikabidhi Ofisi Binafsi ya Waziri ya Afya kwa ajili ya kugawiwa kwa watoto wa kike wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Kupitia ofisi binafsi ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya ilikiri kupokea maboksi 100 ya taulo za kike na kuwasilishwa kwa wabunge wa viti maalum katika maeneo husika kwa ajili ya ugawaji.

Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuishukuru kumshukuru Mheshimkwa Naibu Waziri wa Afya, Dr. Godwin Mollel kwa barua yenye Kumb Na. NWAF/JUM/2024/4 kutushukuru kwa mchango wetu katika kuwasaidia watoto wa kike nchini.