Safe Haven Foundation Yakabidhi Taulo za Kike 2,400 kwa Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi Msimbazi Mseto

Katika kufungua mwezi wa Hedhi Salama ambao ni Mwezi Mei, Safe Haven Foundation tumetembelea Shule ya Msingi Msimbazi Mseto iliyopo katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonana na watoto wakike na kuwaelemisha juu ya Hedhi Salama. Sambamba na hili tumefanikiwa kukakabidhi Taulo za Kike (pedi) 2,400 kwa wanafunzi hao.

Tunashukuru kwa wale wote ambao wanaaendela kutuunga mkono katika kufanikisha kuwafikia watoto wengi zaidi.

Unaweza kutuandikia kupitia barua pepe yetu ya: info@safehavenfoundation.or.tz